Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
Matendo 9:17-18
PAULO MSAFIRI DUNIA
Kazi
Mtengeneza mahema, mtume
PAULO MSAFIRI DUNIA
Wakati
MATENDO YA MITUME
PAULO MSAFIRI DUNIA
Kiwango
Kiwango 20
Mbinu
Soma kitabu cha Matendo na barua za Paulo katika Agano Jipya.
PAULO MSAFIRI DUNIA
Kazi
Mtengeneza mahema, mtume
PAULO MSAFIRI DUNIA
Wakati
MATENDO YA MITUME
PAULO MSAFIRI DUNIA
Kiwango
Kiwango 20
Mbinu
Soma kitabu cha Matendo na barua za Paulo katika Agano Jipya.
Story
SEHEMU YA 1 YA 3

Sauli wa Tarso

Paulo mtumwa hakutumia maisha yake ya awali kama Paulo ama kama mtumwa.Alizaliwa katika familia ya Kiyahudi sehemu ya Mediterraniani ya kibiashara ,mji wa Tarso,mojawapo ya miji mashuhuri ya Asia ndogo.Alikuwa kutoka jamaa ya Benjamini na akiwa mdogo alisomea chini ya Gamalieli ,rabii aliyeheshimika.

Alijulikana kama Sauli wa Tarso na mbali na kuwa mpinga ukristo,Paulo akaifanya kuwa kazi yake kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu katika sehemu ya Yerusalemi na zaidi ya Yerusalemi.Alishiriki katika kuua mkristo wa kwanza wakujitolea kufa, Stefano.

Although first Mary and then her fiancé, Joseph, were obedient to God and His will, it could not have been easy. They had to live with the fact that those around them would never likely believe their stories about why she was pregnant before marriage.

SEHEMU YA 2 YA 3

Tajriba ya barabara ya Dameski

Katika mojawapo ya misheni zake za mauaji,Sauli alikuwa njiani kutoka Yerusalemi kuelekea Dameski.Alikuwa na lengo la kuwakamata wafuasi wa Yesu pale Dameski na kuwarudisha Yerusalemi. Akiwa barabarani ,Yesu mwenyewe akamtokezea ndani ya mwanga mkubwa ambao ulimwacha Sauli akiwa kipofu kwa siku tatu.Yesu akamuuliza Sauli kwa nini alikuwa akimtesa.Wakati Sauli aliuliza ni nani alikuwa akimzungumzia,jibu lilikuwa wazi:”Mimi ni Yesu ambaye unamtesa”.

Katika siku zile tatu akiwa kipofu,Sauli alifunga kutoka kwa chakula na maji na akaomba sana Mungu.Kitendo hiki kikambadilisha Sauli kumuamini Kristo.Kuona kwake kulirejeshwa ,msaada ulitoka kwa muumini anayeitwa Anania wa Dameski ambaye alimwekelea mikono na kusema kuwa Yesu amemtuma ili kurejesha kuona kwake na ili aweze kujazwa na roho mtakatifu.Baada ya yeye kuona ,Paulo akabatizwa na Anania wa Dameski.

Alivyobadilika upya,akabadilisha njia zake na kuanza kuhubiri kuwa Yesu wa Nazarethi alikuwa Masihi Myahudi na mwana wa Mungu.Mtume huyu mpya akawa anajulikana kwa jina lake la Kirumi Paulo,na akasambaza ujumbe wa Kikristo katika safari nyingi.

SEHEMU YA 3YA 3

Safari za Kimishenari za Paulo

Paulo akawa wa msaada sana kama mtume na akaanzisha makanisa mingi sana katika Asia ndogo na Uropa katika safari zake tatu za Kimishenari.Kwa kuwa alikuwa Myahudi na mwenyeji wa Roma,Paulo aliweza kutumia hali hii ili kuwafikia Wayahudi na wenyeji wa Roma na ujumbe wa kikristo.Aliishi maisha yake vema akiwaambia watu wa kila utamaduni na ukoo kuhusu Yesu ambaye alibadilisha maisha yake kabisa.

Sasa kwa kuwa umeijua hadithi ya Paulo, jaribu ujuzi wako kwake kwa kucheza mchezo.Waweza kujifunza zaidi kuhusu Paulo kwa kusoma kuhusu umahiri wake katika kitabu cha Matendo na pia kwa kusoma barua ambazo aliandika ambazo zimenakiliwa katika vitabu vingi vya Agano Jipya.

Bofya HAPA kupakua mchezo.