Petro akamjibu, akasema, "Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji”
Akasema, “Njoo,”
Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Matayo 14:28-29
PETRO MWAMBA
Kazi
Mvuvi, mtume
PETRO MWAMBA
Wakati
MATENDO YA MITUME
PETRO MWAMBA
Kiwango
Kiwango 18
Mbinu
Soma Injili nne, Kitabu cha Matendo ya Mitume, na Barua za Kwanza na Pili za Petro.
PETRO MWAMBA
Kazi
Mvuvi, mtume
PETRO MWAMBA
Wakati
MATENDO YA MITUME
PETRO MWAMBA
Kiwango
Kiwango 18
Mbinu
Soma Injili nne, Kitabu cha Matendo ya Mitume, na Barua za Kwanza na Pili za Petro.
Story
SEHEMU YA 1 YA 3

Hisia

Petro alikuwa mzuri katika mambo mengi lakini kukanya hisia zake halikua mojawapo ya hayo mambo. Ingawa alimpenda Yesu sana, Petro alikuwa mwanafunzi ambaye alikuwa na hisia, alikuwa anakimbilia kutenda jambo bila kufikiria. Petro angekuwa mwema katika timu lakini pia mara ingine angemkosea Yesu.

Lakini Yesu alimpenda Petro na aliona uwezo wake wa kuwa kiongozi. Yesu alimsamehe Petro, hata alipokosea kikweli na akampa changamoto mwanafunzi wake mwenye nia thabiti kuwatunza wale ambao wangekuja kumwamini.

Petro alipojitiisha kikamilifu kumfuata Yesu, alitumiwa kwa nguvu kumtumikia Mungu akiwa mmoja wa mitume mashuhuri zaidi. Kuna tumaini kwa kila mtu kama watamfuata Yesu!

SEHEMU YA 2 YA 3

Kujifunza Juu ya Kazi

Petro alitoka Bethsaida, kijiji cha wavuvi kwenye pwani ya kaskazini-mashariki ya Bahari ya Galilaya. Yesu alipomwomba Petro amfuate, mvuvi alitupa tu nyavu zake na kumfuata. Petro alijitolea kwa bidii kwa ajili ya safari iliyokuwa mbele yake, hata iweje.

Petro alijitokeza kati ya wanafunzi wa Yesu kwa shauku yake. Mara moja katikati ya dhoruba alimwona Yesu akitembea juu ya Bahari ya Galilaya kuelekea wanafunzi, ndiye pekee aliyekuwa na ujasiri na azimio la kumwomba Yesu kama angeweza kutembea nje na kukutana Naye. Yesu alikubali na Petro aliweza kutembea juu ya maji mpaka akakengeushwa na dhoruba na kuanza kuzama. Lakini Yesu alikuwepo ili kumwokoa. Alikuwa daima.

SEHEMU YA 3YA 3

Mtu wa Vitendo

Petro alimlinda sana Bwana wake na akamkata sikio mtumishi wa kuhani mkuu aliyekuwa katika kundi lililotumwa kumkamata Yesu kabla ya kuuawa kwake. Yesu alimwonyesha Petro kwamba jeuri haikuwa jibu kwa kuponya sikio la mtu huyo mara moja.

Hofu ya Petro ilipomzidi, alifuata shambulio lake kwa mtumishi huyo kwa kumsaliti Yesu, akikana mara tatu kwamba yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa bwana Wake baada ya Yesu kukamatwa. Lakini Yesu hata alisamehe tendo hilo la woga. Baada ya kufufuliwa kutoka kwa wafu, Yesu alizungumza na Petro na kuona toba ya mwanafunzi wake akamwomba awachunge “kondoo” wake—wale ambao wangemwamini.

Kwa sifa ya Petro, alikubali nafasi ya pili na maisha ya pili ambayo Yesu alitoa. Aliendelea kuwa kiongozi mwenye nguvu sana katika kanisa la kwanza, akishiriki habari njema ya Yesu na yeyote aliyekutana naye. Petro aliendelea kujitolea kwa Yesu maisha yake yote.

Sasa kwa kuwa unajua hadithi ya Petro, jaribu ujuzi wako kuhusu yeye kucheza mchezo. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu Petro kwa kusoma masimulizi ya injili ya wakati wake na Yesu katika vitabu vya Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Jifunze zaidi matukio yake katika kitabu cha Matendo. Unaweza pia kusoma barua zake zilizorekodiwa katika vitabu vya I na II vya Petro.

Bofya HAPA kupakua mchezo.